ARIS MZUMBE - Mfumo wa Taarifa za wanafunzi Chuo Kikuu cha Mzumbe
ARIS MZUMBE ni mfumo wa taarifa za wanafunzi wa chuo Kikuu cha Mzumbe. Wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hiki wanaweza kutumia mfumo wa ARIS unaopatikana katika mtandao. Mfumo huu unawawezesha wanafunzi na wafanyakazi wa chuo Kikuu cha Mzumbe kufanya baadhi ya mambo yanayohusu chuo mtandaoni. Wanafunzi wanaweza kufanya usajili wa kozi kuangalia maemdeleo ya masomo yao katika mtandao huu. Walimu na Wafanyakazi wengine wanaweza kuweka masomo, kuangalia idadi ya wanafunzi kulingana na kozi husika na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi. Mambo mengine yanayopatinkana ARIS ni kama kufuatilia makazi/hostel na kufanya malipo Ku - Log in Mzumbe Aris Link za Ku log in ziko hapo chini. Kumbuka: Username ni namba yako ya usajili mfano 31302493/T.17 na password ni jina lako la ukoo lililoandikwa kwa herufi kubwa. ukifanikiwa ku log in kwa mara ya kwanza hakikisha unabadilisha neno la siri ili isiwe rahisi mtu kujaribu kuingia katika akaunti yako bila ruhusa. Kama umekutana na tatizo lolote l...