Chuo cha Madini Dodoma - Mineral Resource Institute ( MRI- Dodoma )



Chuo cha Madini Dodoma - Mineral Resource Institute ( MRI- Dodoma ) ni taasisi ya Sayansi ya Dunia (Earth Science) ambayo ilianzishwa na wizara ya Madini Dodoma Agosti 1982. Taasisi imesajiliwa na NACTE chini ya wizara ya Elimu Tanzania.
Chuo kinapatikana Jijini Dodoma eneo la Mbwanga, kata ya Miyuji pembeni kidogo ya barabara ya Arusha na karibu zaidi na Chuo cha Mipango. Chuo hiki ni moja kati ya vyuo bora Tanzania vinavyotambulika kwa kutoa wataalamu bora katika sekta ya madini. Kuangalia matokeo yaliyopita angalia HAPA

Mawasiliano ya Chuo cha Madini Dodoma

Chuo cha Madini

S.L.P 1696
Dodoma – Tanzania

Simu:

+255 (0) 26-2300472
+255 (0) 26-2303159

Mitandao ya kijamii

Facebook

Kozi zinazotolewa

  1. Ordinary Diploma in Geology and Mineral Exploration
  2. Ordinary Diploma in Petroleum Geosciences
  3. Ordinary Diploma in Mining Engineering
  4. Ordinary Diploma in Mineral Processing Engineering
  5. Ordinary Diploma in Environmental Engineering and Management in Mines
  6. Ordinary Diploma in Land and Mines Surveying

Vigezo vya kujiunga

Vigezo vya kujiunga ni vilevile vinavyotolewa na NACTE. kwa kutembelea tovuti ya NACTE unaweza kuvifahamu vigezo hivyo ulingana na mwaka husika.

Jinsi ya kujiunga

Application hufanyika kuanzia mwezi Agosti kila mwaka kwa kujaza fomu kuanzia mwezi Machi. Application zote inabidi zitumwe kwa Mkuu wa chuo kabla ya Mei 10. Fomu zitapatikana chuoni madini, Taasisi ya jiolojia - TanzaniaGeological Survey of Tanzania (GST), ofisi zote za madini za mikoa na nchi na wizara ya Madini.
Wanafunzi watakaochaguliwa ni 150-200 kwa awamu ya kwanza. Kuna uwezekano wa kuwa na awamu ya 2 na ya 3 kutegemeana na mwaka husika. Waliochaguliwa kujiunga wataruhusiwa kubadilisha kozi ndani ya wiki 2 za usajili tu.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Chuo cha Mipango Dodoma - Institute of Rural Development Planning (IRDP)

UDOM SR - Mfumo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma